Na.Yuster Sengo
Halmashauri ya wilaya ya Ulanga imepongezwa kwa juhudi za kuhifadhi misitu kwa kupanda miti ya asili na miti ya kisasa kwani inasaidia katika kuleta mvua ambayo maji yake yanachangia kwa asilimia kubwa kwenye mradi wa uzalishaji wa umeme wa mwl.Nyerere hydropower
Akizungumza wakati wa kutembelea banda la Halmashauri ya wilaya ya ulanga katika maonesho ya nane nane yanayofanyika katika viwanja vya Mwl Julius Kambarage Nyerere ,Mkuu wa Wilaya ya pangani Mh. Ghalib Lamsema kuwa ni vizuri kuendelea kuhifadhi misitu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya Nchi
Hata hivyo mkuu wa Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Bw. Juma Kapilima akifafanua wakati wa kukagua banda hilo amesema kuwa Wilaya ya Ulanga imebarikiwa kuwa na miti mingi ya kupanda pamoja na ya asili ambayo kwa pamoja miti hiyo inaleta matokeo mazuri
Aidha ameongeza kuwa Wilaya ya Ulanga inajihusisha na kilimo cha kokoa,Mpunga, Migomba ,Karanga ambapo mazao hayo yanastawi vizuri kutokana na hali ya hewa inayopatikana wilayani humo
‘’Hapa kuna bidhaa mbali mbali kama vile mchele,mahindi ,ndizi,choroko na kunde,bidhaa zote hizo zinalimwa Wilaya ya Ulanga na zinastawi vizuri sana “Amesema Bw.Kapilima
Akizungumzia bidhaa nyingine Bw. Kapilima amesema kuwa kuna nyungo zinazo tengenezwa Ulanga ambazo zina ubora mkubwa pamoja na vyungu ambavyo vinapatikana Ulanga na vinaukubwa tofauti tofauti
Ikiwa leo ni siku ya kwanza ya Maonesho ya nane nane jumla ya taasisi 18 zimetembelewa na wakuu wa Wilaya ambao ni Mh.Ngollo Malenya kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga na Mh.Ghalibu Lingo wa Halmashauri ya Pwani .
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.