Na.Yuster Sengo
Bidhaa ya mkaa mbadala inayotengenezwa kwa kutumia makaratai imekuwa kivutio kwa watu wengi wanao tembelea Banda la Ulanga kwenye maonesho ya nane nane yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Mkoani Morogoro
Akizungumza wakati wa maonesho hayo Bw.Jonas Tumsime Jason ambaye ni mtengenezaji wa mkaa mbadala amesema kuwa kwa kutumia mkaa huo tunatunza mazingira pamoja na misitu yetu ambapo kwa Wilaya ya Ulanga kwa kutunza misitu tunapata kiasi kikubwa cha mvua kinacho tiririsha maji kwenye mto Kilombero na maji ya mto huo unachangia kiasi kikubwa cha maji katika mradi wa Mwl Nyerere Hydropower
“Tunafanya kutengeneza mkaa mbadala kwasababu Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga tuna lengo kubwa la kuhifadhi mazingira ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa maana kwa kukata miti hivyo tunaweza kusababisha ukame wa mvua na kusababisha kukosa maji katika mto kilombero na hivyo kuzorotesha juhudi ya Serikali katika mradi wa Mwl.Nyerere Hydropower”Amsema Bw.Tumsime
“Mkaa mbadala huu unatengenezwa kwa makaratasi na siyo miti kama tulivyozoea,kwahiyo hapa unaweza kuona ni jinsi gani Misitu yetu inavyoweza kutunzwa kwa maana miti haitakuwa ikikatwa tena kwaajili ya kuchoma mkaa”Ameongeza Bw Tumsime
Akizungumzia jinsi ya kutengeneza mkaa huo Bw. Tumsime amesema kuwa ni rahisi sana kutengeneza mkaa huo hata ukiwa nyumbani kwani si lazima kutumia mashine za kisasa kwani unaweza kufinyanga makaratasi hayo kwa kutumia mkono wako na kupata mkaa
Akitaja hatua zinazotakiwa kufatwa kwenye kutengeneza mkaa huo Bw.Tumsime amesema kuwa kitu cha muhimu cha kuwa nacho ni mkaa na maji tu hivyo ni rahisi kutengeneza haka ukiwa nyumbani
“Hatua ya kwanza ni kuchana makaratasi kwa vipande vidogo vidogo na kisha kuviloweka kwa maji hadi kuwa kama uji kwa muda wa siku nne hadi siku saba baada ya hapo unazifinyanga kama tonge la ugali kisha utaanika kwenye jua kwa siku mbili na kuendelea baada ya kukauka utakuwa tayari kwaajili ya matumizi ya kupikia nyumbani”Amefafanua Bw.Tumsime
“Mkaa mbadala huu unaweza kutumika kupikia vyakula mbali mbali ikiwa ni pamoja na chai ,maharage,ugali,wali nk”Ameongeza Tumsime
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.