Ulanga
Na Fatuma Mtemangani
Serikali wilayani ulanga mkoani morogoro imefanikiwa kupungu za Chagangamoto ya ukosefu wa vifaa tiba ikiwemo dawa kupitia huduma ya bima ya afya ya chf iliyoboreshwa.
Akizungumza na ulanga fm ofisini kwake mfamasia wa Halmashauri bwana Jackson Nyamsani amesema kua upatikanaji wa huduma ya chf iliyoboreshwa kwa sasa haina tatizo kutokana na serikali kuleta madawa ambayo yatakidhi matakwa ya watumiaji wa chf katika hospital,vituo vya afya pamoja na zahanati.
Nyamsani amewataka wajumbe walio chaguliwa katika jamii kutoa taarifa kwa wakati pale wapofika katika vituo vya afya na kuhamasisha wananchi kwa kuwapatia elimu juu ya huduma zinazotolewa na bima ya afya chf iliyoboreshwa kwani wao ndiyo sehemu ya jamii.
Aidha ameongeza kua kwa wale wasiojiunga na huduma hiyo wafanye jitihada kwani bima ya afya ya chf iliyoboreshwa ni mkombozi kwa jamii hasa zenye kipato cha chini.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.