ULANGA
NA Fatuma Mtemangani
Viongozi wa ngazi ya vitongoji,vijiji,kata wakiwemo waheshimiwa madiwani wanashauriwa kuhamasisha vijana kwa kuwapatia elimu lika kupitia mikutano yao namna ya kujikinga na mwagonjwa ya zinaa ikiwemo afya ya uzazi na ukimwi.
Akizungumzia suala la magonjwa hayo mratibu wa ukimwi wilayani ulanga bi leah ndama amesema kuwa miongoni mwa kazi zinazo fanywa na idara kwa sasa ni kutoa elimu kwa makundi mawili kuna vijana ambao wako nje ya shule na wale ambao wako ndani ya shule hasa katika masuala ya ukimwi na afya ya uzazi.
Bi.leah amesema kuwa kwa upande wa shule idara imeanzisha klabu za ukimwi kwa shule zote za sekondari wilayani ulanga kwa kutoa elimu mbalimbali kuhusu afya ya uzazi na ukimwi.
Hata hivyo kwa upande wa vijana walio nje ya shule wakiwemo vijana wanaoendesha pikipiki maarufu kama boda boda,wahudumu wa bar na guest,wafanyakazi wa saloon idara inakutana nao na kusikiliza changamoto wanazokutana nazo na namna gani ya kukabiliana nazo.
“Ukiangalia wafanyakazi wa bar kazi yao wanayofanya ni kazi kama kazi nyingine lakini kupitia kazi zao wanachangamoto sasa kupitia zile chnangamoto zao tunaelekezana namna gani wakabiliane kupitia hizo changamoto zao,wajikinge vipi katika suala zima la kupata magonjwa ya ngono na ukimwi na hatimae kupoteza ndoto zao hizo ndiyo miongoni mwa shughuli ambazo huwa tunazozifanya kama idara kupitia kitengo cha ukimwi katika halmashauri ya wilaya ya ulanga”. alisema bi.leah.
“Sambamba na hilo kama idara husimamia shughuli ambazo zinafanywa na wadau mbalimbali katika kupambana na suala la ukimwi na magonjwa ya ngono tuna watu kama shirika la kamfed wao wanashughulika na watoto wa kike kuwahamasisha umuhimu wa elimu kwa kujisomea na kutimiza ndoto zao,shirika la pamoja tuwalee wao nao wana klab mbalimbali za watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kila kijiji pamoja na shirika la solidamed ambao wanawaelimishaji jamii kila kijiji na wale waelimishaji jamii wametengeneza vikundi vyao vya hamasa hivyo wanatoa elimu kwa njia ya sanaa katika maeneo mbalimbali wakiwemo vijana na makundi mbalimbali”.alisema bi. leah
Bi.lea amewataka wadau mbalimbali kupambana hasa suala zima la ukimwi ili ifikapo mwaka 2030 maambukizi ya ukimwi kufikia asilimia sifuri na vifo vitokanavyo na ukimwi na unyanyapaa kufikia asilimia sifuri.
Hata hivyo bi.leah ameelezea changamoto wanazokutana nazo juu ya utoaji elimu ya magonjwa ya zinaa ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya kifedha hali inayopelekea kutoifikia jamii kwa wakati hivyo halmashauri kwa kupitia makato ya ndani wanawafikia vijana.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.