ULANGA
Na Fatuma Mtemangani
Idara ya Mifugo na Uvuvi imefanikiwa kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo kutoa kinga tiba dhidi ya magonjwa ya mifugo ikiwemo ngombe,Mbuzi,Kuku,Nguruwe,Kondoo,Sungura pamoja na Mbwa.
Akizungumzia chanjo hiyo Afisa kilimo wlaya ya Ulanga bwana Bernad Ntikabuze amesema kuwa jumla ya chanjo zilizotolewa kwa mifugo ni pamoja na ngombe 18,359,Mbuzi 7,542,Kondoo 6,901,Kuku 41,628,Nguruwe 3,017,Sungura 326,Mbwa 81 mifugo hiyo imepatiwa kinga aina ya ndigana,ndorobo,madini joto,ukurutu pamoja na kuhara damu.
Ntikabuze alisema kuwa idara pia wamefanikiwa kutengeneza vutambulisho kwa wafugaji waliosajili mifugo yao katika kipindi cha mwaka 2016/2017 ambapo jumla ya vitambulisho 1140 vilitengenezwa na kusambazwa kwa wafugaji hivyo katika marudio ya zoezi la utambuzi wa upigaji wa chapa wa mifugo jumla ya ngombe 6571 wamepigwa chapa kati ya hao 3521 wamerudiwa baada ya chapa kufutika na ngombe 3050 ni wapya hali ilyopelekea kufikia jumla ya ngombe 49,636 waliopigwa chapa wilayani Ulanga na zoezi hilo bado linaendelea katika maeneo mbalimbali.
Pia idara inasimamia shughuli za minada ya mifugo ambapo jumla ya ngombe 2,178 Mbuzi 1,800,Kondoo 1,1018 waliuzwa mnadani pamoja na ufuatiliaji wa matukio ya magonjwa ya mifugo vijijini hivyo idara imegundua kuwa kuna dalili za kuwepo kwa ugonjwa wa midomo na miguu{FMD}katika vijiji vya Nakafulu,Iragua,Igota,Mavimba na Kivukoni.
Kwa upande wa Halmashauri imefanya jitihada za kutoa elimu na ushauri kw wafugaji ambapo jumla ya wafugaji 18,931 wamepatiwa elimu na ushauri juu ya ufugaji bora wa mifugo na uhifadhi wa malisho kwa matumizi endelevu kupitia njia mbalimbali kiwemo Redio Ulanga Fm,mikutano ya wafugaji vipeperushi pamoja na majarida.
Pia kuboresha maeneo ya malisho,kuzingatia kinga na tiba dhidi ya magonjwa,kushiriki zoezi la kupiga chapa na uchangiaji wa ujenzi wa miundombinu ya mifugo kama vile majosho,malambo,visima,mabirika na mapalio.
Aidha idara inasimamia shughuli za utoaji wa leseni ya uvuvi na ukusanyaji na kufanikisha kutoa leseni 107 zenye thamani ya shilingi 4,280,000/= na ushuru wa samaki ni shilingi 1,432,500/= jumla kufikia shilingi 5,712,500/=.
Idara pia ina mikakati ya kuendeelea kutoa elimu kwa wafugaji ili waweze kutumia mbegu bora za mifugo kwa ajili ya kuzalisha mazao bora na yenye tija ambayo itapelekea kujikwamua kiuchumi,kufanya usajili wa mifugo wakati wa kiangazi ili kupata idadi kamili ya mifugo kwa wilaya ya Ulanga,kutambua maeneno ya malisho yaliyotengwa,kuhamasisha wafugaji kushiriki ipasavyo katika kuchangia ujenzi wa miundo mbinu ya mifugo na kuanzisha miradi ya unenepeshaji.
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.