Ulanga
Na Fatuma Mtemangani
Halmashauri wilayani ulanga mkoani Morogoro imefanikiwa kupunguza uharibifu wa mazingira ikwemo uchomaji moto misitu,vyanzo vya maji,ukataji kuni,uchomaji wa mkaa pamoja na kutenga maeneo ya malisho.
Akizungumza na Redio Ulanga Fm afisa misitu wilaya ya Ulanga bwana Melkizedek Bosco amesema kua kwa sasa halmashauri kwa kushirikiana na mradi wa kupambana na uharibifu wa mazingira Kilorwemp wamefanikiwa kuaandaa sheria ndogo za mazingira kwa kila halmashauri za vijiji.
Bwana Bosco ameongeza kua mpaka sasa tayari sheria hizo zimeshapitishwa na wana kamati katika vijiji husika na kinachosubiriwa ni kupelekwa kwenye baraza la madiwani ili shughuli za uvunaji misitu kupitia vijiji husika viweze kunufaika kupitia misitu yao.
Vijiji ambavyo tayari vimepitisha sheria hiyo ni pamoja na kijiji cha Kichangani,kijiji cha Idunda na kijiji cha Libenanga.
Mradi wa Kilorwemp unafanyakazi kati wilaya tatu nchi ikiwemo wilaya ya Ulanga,Kilombero pamja na Rufiji kwa lengo la kupambana na uharibifu wa mazingira
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.