ULANGA
Na Fatuma Mtemangani
Afisa misitu wilayani ulanga mkoani morogoro bwana Alfan Misayo amewapongwzawananchi wa wilaya ya ulanga kwa hatua nzuri ya utunzaji wa mazingira hivyo amewataka kupanda miti kwa wingi na kukata vibali vya uvunaji wa miti ili kutunza mazingira kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Bwana Misayo alisema kuwa kwa sasa uoteshaji na ukuzaji wa miti ni biashara kwa taifa letu hivyo wananchi wanapaswa kutumia fursa hii ili kujiongezea kipato ndani ya familia na jamii kwa ujumla.
Katika hatua nyingine bwana Misayo amesema kuwa amempongeza mtoto Grigori Bilauri mkazi wa kijiji cha uponera wilayani ulanga kwa kumiliki vitalu viwili vya miche vyenye jumla ya miche 1,700 ambavyo amevitengeneza kwa nguvu zake mwenyewe kwa lengo kujipatia kipato na kutunza mazingira kwa wilaya ya ulanga.
Hata hivyo kama idara wameahidi kumpatia elimu zaidi motto Grigori juu ya utunzaji na uendelezaji wa miche hiyo ili iweze kumkwamua kiuchumi.
Mtoto Grigori Bilauri aliyehitimu elimu darasa la saba mwaka 2016 ambaye hakuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari ameamua kujishughulisha na kazi hiyo kwa lengo la kujiongezea kipato huku akikiri kukosa elimu ya kutosha ya uendeshaji wa miche hiyo.
Bwana Misayo amewata wananchi wote wanaojihusisha na uvunaji wa miti kutuma maombi ya upatikanaji wa vibali ili kuondoa usumbufu utakaojitokeza hali itakayowafanya kufanya kazi ya uvunaji wa misitu kisheria ambapo zoezi hilo litafikia kikomo mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka 2018.
Hivyo ameelezea changamoto wanazokutana nazo juu ya utoaji elimu kwa jamii ni pamoja na ukosefu wa watumishi katika idara ya misitu,miundo mbinu ya kifedha hali inayopelekea kutoifikia jamii kwa wakati hivyo.
“Kuanzia sasa tutafuata sheria za mazingira kama zinavyoelekeza kwa yeyote atakaekiuka kukata miti hovyo,kuchoma mkaa,kuharibu vyanzo vya maji pamoja kupasua mbao ndani ya misitu atatozwa faini ya shilingi …..hivyo kila mwananchi anapaswa kulinda misitu iliyo karibu yake na kuzingatia ushauri wanaopewa na wataalam wa misitu ili kusaidia kizazi cha sasa na cha baadae”.alisema bwana misayo.
Sambamba na hilo ameitaka jamii kutobweteka kwa kufanya vizuri utunzaji wa misitu kwa mwaka hivyo jamii inatakiwa kuishi kwa kufuata sheria na kanuni bora juu wa utunzaji wa misitu.
mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.