Na patrick mishomari
Mgogoro wa shamba la karanga miti lenye ukubwa wa hekali elfu 49 ni moja kati ya mashamba poli yaliyo orodheshwa kati ya mashamba poli ya wilaya ya ulanga mkoani morogoro.
Akijibu swali la diwani wa minepa Michael Mahiringa katika baraza la madiwani ,mwenyekiti wa baraza hilo mh.furaha lilongeli aliye taka kujuwa shamba la karanga miti ni lawanakijiji wa chikuti au la mwekezaji .
Mh.Furaha Lilongeli amesema shamba hilo lilikuwa na muwekezaji lakini walipokea maelekezo ya kuyatambua mashamba pori na liliandikwa kama shamba pori na waliiomba wizara ya ardhi shamba hilo lirudi mikononi mwa wananchi wa chikuti na jitihada hizo zilizaa matunda kwakumleta waziri wa ardhi william lukuvu katika halmashauri ya wilaya ya ulnga na kufanya naye mkutano katika kijiji hicho.
Pia lilongeli ameongeza kuwa mkutano huo walikubaliana kuwa hekali hizo elfu 49, hekali elfu 40 zibaki kwa mwekezaji na hekali elfu 9 zirudi kwa wananchi lakini mpaka sasa bado hekali hizo hazijakabidhiwa kwa wananchi wa kijiji cha chikuti.
“Halmashauri ninayo iyongoza pamoja na madiwani kwa baraza lililo pita walimuagiza mkurugenzi na mtalaamu wa afisa ardhi kwenda wizara ya ardhi kuulizia mchakato wa kugawa hizo hekhali elfu tisa lini utafanyika lakini majibu yamerudi tofauti na makubaliano kwenye kikao na waziri katika kikao chikuti najibu lilikuwakwamba zikitolewa hizo hekali kwa mikataba ya kukodishwa kwa wananchi “amesema lilongeli.
Kwa upande wa mbunge wa wilaya ya ulanga mh.Goodluck Mlinga ameongeza kuwa shamba hilo ni pori na ilihizinishwa na nyanganywa mwekezaji huyo lakini aliomba arudishiwe na akapewa afanye kazi ndani ya miezi 18 ila bado haja fanya kazi yoyote mpaka sasa.
Mh.Mlinga amemtaka diwani wa minepa Michael Mahilinga kuambatana na timu ya watu 20 kwenda kuweka kambi bungeni dodo kwaajili ya kuonana na waziri ili kupata ufumbuzi wa mgogoro unao endelea katika kijiji hicho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.