Ulanga
Wanawake wilayani Ulanga Mkoani Morogoro uenda wa kakuwa zaidi kiuchumi na kupunguza vitendo vya ukatili dhidi yao endapo wataungana na kulitumia vyema jukwaa la wanawake litakalozinduliwa hivi karibuni.
Mohamedi Atiki ni afisa maendeleo ya jamii wilayani Ulanga amesema kua uwepo wa jukwaa hilo utasaidia kuwaunganisha wanawake na kuibua fursa za kiuchumi na namna sahihi ya kupambana na vitendo vya ukatili dhidi yao.
Bwana Atiki ameongeza kua wanawake wana nguvu kubwa ya kusimamia masuala ya maendeleo lakini wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kutozitambua fursa zilizopo katika maeneo yao,kukatishwa tama na baadhi ya wanaume,kudhurumiwa,kutopewa nafasi katika kusimamia mirathi pamoja na kukosa sauti ya pamoja ya kutekeleza haki zao.
Hata hivyo katika kukabiliana na changamoto hizo ofisi ya maendeleo ya jamii imeandaa mkakati wa kuwatumia wataalamu kutoka taasisi za kifedha ikiwemo benki na taasisi mbalimbali za maendeleo ili kuelimisha umma wa wanawake juu ya masuala ya maendeleo.
Jukwaa la wanawake linatarajia kuzinduliwa rasmi wilayani Ulanga tarehe 27/4/2017 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali lililotolewa na makamu wa rasi Samia Suluhu Hassani la kutaka kila wilaya kuunda jukwa la wanawake.
Na Fatuma Mtemangani
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.