KAIMU KATIBU TAWALA WA MKOA WA MOROGORO NDUGU GERADI HAULE AMEITAKA TAMISEMI KUWAPELEKA MAAFISA TEHAMA NA MAWASILIANO KATIKA KILA HALMASHAURI NCHI.
NDUGU HAULE AMEYABAINISHA HAYO HII LEO KWENYE UZINDUZI WA MAFUNZO YA TOVUTI KWA MAOFISA HABARI NA TEHAMA WA HALMASHAURI NA MIKOA YA MOROGORO, KILIMANJARO, ARUSHA NA TANGA YALIYOANZA TAREHE 20/3/2017 NA KUMALIZIKA TAREHE 27/3/2017 KATIKA UKUMBI WA EDEMA MKOANI MOROGORO.
MAFUNZO HAYO YAMEANDALIWA NA MRADI WA USAID WA WATU WA MAREKANI KWA KUSHIRIKIANA NA TAMISEMI YAMEFANYIKA KATIKA MIKOA MITANO IKIWEMO MIKOA YA MBEYA,KIGOMA,MTWARA,MOROGORO PAMOJA NA DODOMA AMBAKO UZINDUZI HUU UMEFANYIKA KITAIFA.
PIA AMEISHUKURU SERIKALI KWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA MAFUNZO HAYO NA KUWATAKA WATENDAJI KUWAPA USHIRIKIANO KWENYE SUALA LA UWAZI KATI YA SERIKALI NA WANANCHI KWA KUWAPA KIPAU MBELE KWA KUTOA MREJESHO KWENYE SERIKALI YAO.
KAIMU KATIBU TAWALA WA MKOA AMEONGEZA KUA TOVUTI HIZI ZINAWEZA KUIPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KWA MATAIFA MENGINE NA KULETA MAENDELEO KUPITIA SERIKALI HII YA UCHUMI NA VIWANDA KWA TAIFA.
KWA UPANDE WAKE MSIMAMIZI WA MAFUNZO HAYO BWANA DAUD OLE LAPUTI AMESEMA KUA KUPITIA ,MAFUNZO HAYO MAAFISA HAO WATAFANYA KAZI KWA WELEDI ILI KUFIKIA MALENGO YA SERIKALI NA MRADI HUO KWA KULETA UWAZI KWA WANANCHI.
DAUD LAPUTI AMEONGEZA KUA TOVUTI HIZI ZITASAIDIA KUWEKA TAARIFA ZAKE ZA UWAZI NA KWA WAKATI ILI ZIWEZE KUWASAIDIAWANANCHI KUJUA TAARIFA KWA WAKATI NA KUTOA MALALAMIKO,MAONI PAMOJA NA KERO ILI ZIWEZE KUFANYIWA KAZI.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.