JUMLA YA VIJANA ISHIRINI WA SHULE YA SEKONDARI KWIRO WILAYANI ULANGA MKOANI MOROGORO WAMETUNIKIWA VYETI BAADA YA KUTUMIKIA SCOUTI KWA MUDA WA MIAKA MIWILI WAKIWA SHULENI HAPO.
VIJANA HAO WAMESEMA KUWA WAMEPATA MAFANIKIO MENGI KWA KUTUMIKIA SCAUTI WAKIWA SHULENI IKIWA NI PAMOJA KULINDA AMANI NA UTULIVU KATIKA SHULE HIYO PAMOJA NA KUPATA ELIMU YA KUJITEGEMEA KWA KULIMA MBOGAMBOGA AMBAZO ZIMEWASAIDIA KUJIENDESHA NA SCAUTI.
MGENI RASMI KTIKA ZOEZI HILO LA UTOAJI VYETI NI KATIBU WA UMOJA WA VIJANA CCM UVCCM BI RUKIA MAKOJA NA AMEWATAKA VIJANA HAO BAADA YA KUHITIMU MASOMO YAO WAENDELEZA SCAUTI POPOTE WAENDAKO KWANI WATAKUWA WAMEENDELEZA UZALENDO WA NCHI.
BI MAKOJA AMEWATAKA VIJANA HAO KUTUMIA ELIMU WALIYOIPATA SHULENI HAPO KUITUMIA VIZURI ILI KUEPUKA MATATIZO YA UHALIFU NA WATU AMBAO WATATAKA KUWATUMIA VIBAYA KWA KIPINDI WATAKAPOHITIMU MASOMO YAO.
AIDHA AMEWATAKA VIJNA HAO KUWA WABUNIFU NA KUTEKELEZA MALENGO WALIYOJIWEKEA NA KUTIMIZA MALENGO YAO WALIOJIWEKEA ILI WAWEZE KUTIMIZA NDOTO ZAO.
MWISHO
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.