Zaidi ya kaya 50 zimejiunga na mfuko wa bima ya afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa katika uzinduzi wa zoezi la uandikishaji wa kaya kwa kaya uliofanyika katika kata ya Minepa wilayani Ulanga.
Hayo yalisemwa na Meneja (CHF) wilaya Bi Sigirinda Mdemu wakati wa ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji kaya kwa kaya kwa mwaka 2017 ambapo alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuongeza idadi ya wanachama hadi kufikia asilimia 80 ambayo ni lengo lililokusudiwa.
Aidha katika uzinduzi huo pia walishiriki viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo watendaji wa vijiji, wenyeviti wa vijiji na vitongoji ambao kwa pamoja waliadhimia kufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na maafisa waandikishaji katika maeneo yao.
Hata hivyo baadhi ya wananchi walihoji juu ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya vya serikali ikiwemo zahanati na hospitali za wilaya na kuongeza kuwa hali hiyo imekuwa ikiwakatisha tamaa ya kujiunga na huduma hiyo.
Akitoa ufafanuzi Dkt. Nataria Mtolela ambaye ni dakatri mshauri wa mradi humo ameeleza kuwa kwa sasa dawa aina nyingi zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya tofauti na zamani sababu maboresho mengi yamefanyika kuhakikisha madawa yanapatikana kwa wanachama wote
Vilevile Dkt. Mtolela alitoa wito kwa wananchi kujiunga na bima hiyo ili kupunguza gharama za matibabu na kwasasa wananchama wote waliojiunga watapata huduma katika mkoa wa Dodoma, Morogoro na Shinyanga tofauti na awali ambapo mwanachama alikuwa akihudumiwa sehemu aliyojiunga tu.
Chf iliyoboreshwa imezindua kampeni ya uandikishaji wa wanachama wapya kwa kupita kaya kwa kaya ili kuhakikisha wananchi wote wanajiunga na wanapata huduma bora za afya kwa gharama ya Tshs. 10,000 kwa mwaka mzima kwa wanafamilia sita.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amehaidi kutoa shilingi milioni moja kwa kijiji ambacho kitaongoza kwa kuandikisha wananchama wengi wa Mfuko wa Afya ya Jamii.
Aliyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wananchi wa tarafa ya Mwaya katika uwanja wa Shule ya Msingi Mwaya ikiwa ni uzinduzi wa uhamasishaji wa uandikishaji wa wanachama kimkoa.
Alisema kuwa viongozi wa ngazi zote ndani ya Wilaya ya Mkoa wanapaswa kushikamana katika kufanikisha zoezi la uandikishaji wa wanachama ili kuhakikisha wananchi wote wanajiunga na bima ya Afya ya Jamii kwaajili ya kupata uhakika wa matibabu kwa mwaka mzima na kuahidi kutoa milioni moja kwa kijiji kitakachofanya vizuri.
Dkt. Kebwe aliongeza kuwa Wilaya ya Ulanga kwa mwaka jana iliongoza kimkoa katika uandikishaji na hivyo ni jukumu la viongozi wote ndani ya wilaya kuhakikisha wanaungana na kuendelea kuongoza kimkoa na kupandisha asilimia za uandikishaji kitaifa ambapo kwa sasa mkoa umeandikisha wananchi kwa asilimia 8 tu.
Aidha aliwahakikishia wananchi kuwa serikali imelifanyia kazi suala la upatikanaji wa dawa kwa kuongeza bajeti ya Wizara ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba ambapo jumla ya bilioni 250 zilitengwa ili kuhakikisha wananchi wanapata dawa wakati wote kwenye vituo vya kutolea huduma na zahanati.
Hata hivyo aliwaagiza viongozi wote ndani ya wilaya kufanya uzinduzi katika wilaya zao na kuhakikisha wanachama zaidi wanajiandikisha na hadi kufikia desemba asilimia za uandikishaji zifikie asilimia 50.
Uzinduzi wa uhamasishsji wa uandikishaji wa wanachama wa Mfuko wa Afya ya jamii kimkoa ulifanyika katika wilaya ya Ulanga ambapo Mkuu wa Mkoa alikuwa mgeni rasmina viongozi mbalimbali kutoka wilaya ya Ulanga na Malinyi walihudhuria na kaya zaidi ya 200 zilijiunga kwa siku hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.