Na Yuster Sengo
Mkuu wa wilaya ya Ulanga Mh Ngollo Malenya amewataka vinara wanaofanya kazi za uelimishaji vijijini chini ya chama cha wanasheria wanawake TAWLA ,kufanya kazi kwa uadilifu na kuacha kuwa miungu watu na badala yake wawahudimie wanannchi kwa uadilifu na uaminifu
Akizungumza katika zoezi la ugawaji wa baiskeli kwa vinara hao kwaajili ya kufanyia shughuli za uelimisheji ,Mkuu wa wilaya amewataka vinara hao kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ili kutekeleza majukumu yao kwa uhakika
“Mimi ninawaomba nyie mliopewa dhamana mfanye kazi kwa uadilifu ,mkifanya kazi kwa mabavu nitazungumza na mkurugenzi na mwanasheria ili tuone utaratibu wa kuwaondoa katika nafasi hizo”Amesema mkuu wa wilaya Mh .Ngollo Malenya
Aidha mkuu wa program wa chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Mary Richard amewataka vinara hao kuendelea kushirikiana kwa ukaribu na halmashauri pamoja waratibu wa mradi ili kuleta matokeo chanya kwenye elimu ya sheria kuhusu umilikiji ardhi na masuala mengine ya kijamii
Hata hivyo amewataka vinara hao kutunza baskeli wanazopatiwa kwaajili ya usafiri wakati wa kwenda kutoa elimu vijijini
‘Hii ni awamu ya pili ya mradi wetu,nakumbuka katika awamu ya kwanza tuliomba baiskeli ili zitusaidie katika suala la usafiri kwani kwa jografia ya eneo letu kuna sehemu nyingine magari wala pikipiki haziwezi kufika hivyo sasa leo tunawakabidhi baiskeli hizo na tunaomba zikatumike kwa makusidio yaliyo kusudiwa “Amesema Mkuu wa program Bi.Mary Richard
Baadhi ya vinara waliohudhuria zoezi hilo wameshukuru chama cha wanasheria wanawake (TAWLA)kwa kuwapa baiskeli hizo na kuahidi kutumia kama ilivyokusudiwa
“Tunashukuru sana kwa TAWLA kututupati usafiri huu na tunaahidi kuzitunza na kwa suala la kuwa mungu watu alilolizungumzia mkuu wa wilaya ,tunamuahidi kuwa tutafanya kazi kwa uadilifu na tutahudumia wananchi kama inavyotakiwa”Amesema mmoj wa vinara hao
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.