ULANGA
Na
Fatuma Mtemangani
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Morogoro kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania{UWT} Bi Christina Ishengoma amewataka viongozi na wajumbe wa UWT Wilaya ya Ulanga kulinda uhai wa Chama cha Mapinduzi{CCM}kwa kulipa ada,kuongeza wanachama wapya wenye mapenzi mema na chama.
Bi Ishengoma ameyazungumza hayo hivi karibuni katika baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania Wilaya ya Ulanga lililofanyika kwenye ukumbi wa CCM Wilaya amesema kua viongozi wanatakiwa kuitisha vikao vya kisheria na vya dharura ili kukijenga chama na kuandika mihutasari kwa kumkabidhi katibu wa ccm wilaya na taarifa hizo ziende kwa wakati na zenye ukweli.
Hata hivyo ameongeza kua serikali kwa sasa inatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi katika ahadi zake kwa wananchi ikiwemo miundo mbinu ya barabara,afya pamoja na elimu bure kwa watanzania hivyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kuunga mkono mh.raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania mh.dk.john pombe magufuli.
Aidha amewataka Wanawake wa Wilaya ya Ulanga kulima mazao ya biashara kama vile Pamba,Korosho, na Kahawa na waondoe hofu juu ya upatikanaji wa soko kwa mazao wanayolima serikali imefanya jitihada kubwa kuwatafutia masoko na pia kuongeza viwanda kwa ajili ya wakulima.
“Wakati nikiwa Dodoma ambapo ile bajeti kuu ya serikali kwa kweli niliifurahia sana ile bajeti kwa sababu haijawahi kutokea kwa miaka mingine bajeti kuu ikisomwa iwekwe kipaumbele kilimo,sasa nawaagiza mkalime mazao ya biashara kwa kuwa soko la uhakika lipo hivyo msiwe na wasiwasi juu ya soko kwa Rais wetu anatupenda na ndiyo maana anapambana kwa ajili yetu”alisema Ishengoma.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.