Na Yuster Sengo
Afisa lishe wilayani ulanga mkoani morogoro Bi Rehema kilungi ameeleza mikakati na mipango kazi juu ya utekelezaji wa swala zima la lishe kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano wilyani humo.
Akizungumza wakati wa kikao cha ndani cha halimashauri chenye lengo la kutokomeza utapia mlo kwa watoto na kuendelea kutoa elimu kwa wakina mama wajawazito juu ya kuzingatia matumizi sahihi ya elimu itokanayo na utapia mlo kwa wakina mama wajawazito na watoto.
“Wakina mama wajawazito tujitahidi sana kuzingatia matumizi sahihi ya elimu hii ambayo tunaitoa ili tuweze kuwaokoa watoto zetu na janga hili la utapiamlo”Amesema Bi.Rehema
Hata hivyo nae mratibu wa mradi wa lishe endelevu wilayani ulanga Bw Christofa Jofrey ameongeza kuwa kwa upande wa wilaya ya ulanga maradi umeweza kuendesha mafunzo kwa maafisa ugani kwa kila kata kwa uapande wa kilimo namifungo na kwa ngazi ya halimashauri pia mradi umeweza kusaidi katika kuhamasisha maswala mazima ya lishe hasa kupita kamati za lishe na kwa kila mototo aliye na umri chini ya miaka mitano apangiwe shilingi elfu moja.
Sambamba na hayo Bi kilungi ameitaka jamii na wazazi kwa ujumla kubadilika na kuhakikisha wanajitahidi katika kuzingatia elimu juu ya swala zima utapia mlo kwa watoto nakufikia katika vituo vya afya kwa wakati ili kupatiwa matibabu endapo motto au mama mjamzito ataonekana ana matatizo ya upungufu wa damu au utapia mlo.
Mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.