Na.Yuster Sengo
Wakulima wilayani ulanga mkoani morogoro wametakiwa kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo ili kuepusha tatizo la kuhama hama kufuata ardhi yenye rutuba wakati wa maandalizi ya shamba .
Hayo yamesemwa na kaimu afisa kilimo Bwana Joseph Mkude wakati akizungumza na ulanga fm ,ambapo ameeleza kuwa wakulima wengi wamekuwa na tabia ya kutowatumia wataalamu wa kilimo kwa kufuata kanuni na taratibu za kilimo hali ambayo imesababisha ardhi kupoteza rutuba.
Aidha bwana Mkude ametoa ushauri kwa wakulima kuwa endapo hali ya mazao yao yataonyesha kutokuwa na rutuba wanatakiwa kuwaona wataalamu wa kilimo ,na endapo kutakuwa na ulazima wa kutumia mbolea watashauriwa aina ya mbolea ya kutumia katika mazao haya.
“Niwashauri wakulima pale mazao yanapokuwa siyo bora ni muhimu sana kuwaona wataalamu wa kilimo iliwaweze kuwapa ushauri wa kitaalamu nini cha kufanya ili kuweza kupata mazoa yenye rutuba na ubora unaotakiwa “Amesema Mkude
Hata hivyo bwana mkude amewatahadharisha wakulima kuacha tabia ya kutumia mbolea bila kufuata ushauri wa wataalamu hao kwani inawezekana mbolea inayo takiwa kutumika katika mazao hayo sio ambayo mkulima anaitumia na hvyo kusababisha madhara mengine.
Bwana mkude ametoa wito kwa wakulima kuacha tabia ya kulima kwa mazoea badala yake wawatumie wataalamu wa kilimo kupata maelekezo na kanuni za kilimo.
“Wakulima mnatabia ya kulima kwa mazoea ,tabia hiyo muiache maana mnasababisha kupata mazao yasiyo bora au wakati mwingine kukosa kabisa hivyo ni vizuri kuwatumia wataalam wa kilimo ili kujua mlime mazao gani na kwa wakati gani au hata mtumie mbolea ipi kwa mazao yapi “Amesema Bw. Mkude
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.