ULANGA
Na
Fatuma Mtemangani
Wakulima wa zao la mahindi wilayani Ulanga Mkoani Morogoro wameaswa kuzingatia kanuni bora za kilimo cha kisasa na chenye tija ili waweze kupata mazao ya kutosha.
Hayo yamebainishwa na kaim Afisa Kilimo Wilaya ya Ulanga Bwana Joseph Mkude wakati akizungumza na Rediou Uanga FM walipo mtembelea ofisini kwake amesema kuwa wakulima wanapaswa kutumia mbolea ya kupandia kwa kwa sasa kuboresha zao hilo.
Aidha Bwana mkude ameongeza kua wakulima wanatakiwa kuzalisha zao hilo kwa wingi kwani kwa sasa zao hilo limekuwa ni zao la biashara katika wilaya hiyo na hakuna usumbufu wa kupata soko la uhakika kwani kipo kiwanda cha kutengeneza sembe kilichopo tarafa ya mwaya kijiji cha mbuga na kipo hatua ya mwisho kukamilika.
Bwana.mkude amewataka wauzaji wa mbolea katika maduka ya pembejeo kuuza mbolea hizo kwa bei elekezi iliyopangwa na serilikali ambapo kila mfuko wa kilo hamsini uuzwe kwa bei ya sh.elfu hamsini kwa mbolea aina ya Dap na mbolea ya Yulea iuzwe kwa bei ya sh.Elfu thelathini na tisa kwa kilo hamsini na si vinginevyo.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.