Ulanga
Na
Fatuma Mtemangani
Wananchi wa wilaya ya Ulanga mkoa wa Morogoro wameshauliwa kuwatumia wataalamu wa majengo kukagua maeneo yao kabla ya kuaanza ujenzi ili kuongeza ubora wa majengo hayo.
Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mbagula Bw. Fabian Fabian Likoko wakati alipotembelea kukagua eneo ambalo litakalojengwa ofisi ya kijiji hicho amewapongeza viongozi wa kijiji cha Mbagula kwa kuona umuhimu wa kuwatumia wataalamu wa majengo.
“Nawapongeza sana viongozi wa vijiji kwa kuwatumia wataalamu wa majengo hii inaonyesha kuwa mnataka kuwa na majengo yenye ubora hivyo mnatakiwa kutoingiza mambo ya siasa kwa sasa fanyeni kazi za maendeleo kwa ajili ya wananchi wenu”Alisema Likoko.
Bwana Likoko amesema kuwa ili nyumba iwe bora na ya kudumu ni muhimu kuwatumia wataalam wa majengo kabla ya ujenzi ili kuelekeza namna ya ardhi iliopo ikiwemo , kutoa ushauli na ujenzi upi unafaa katika eneo husika.
Hata hivyo bwana Likoko amefurahishwa na amewapongeza viongozi wa kijiji hicho kwa kumpeleka eneo hilo na kujionea pamoja na kuchukua vipimo kwa ajili ya kuanza ujenzi hivyo taarifaa ya vipimo itakaporudi kijiji kitaendelea na hatu zitakazofata.
Aidha kwa upande wake M/kiti wa kijiji hicho bwana Credo Mbalachi amemshukuru mtaalam huyo wa majengo kukagua eneo hilo kwani ndicho kilichokuwa kinasubiriwa na kwa sasa maandalizi yote yamekamilika ikiwemo nguvu kazi,tofali,pamoja na mawe kwa ajili ya kutimiza ujenzi huo.
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.