ULANGA
NA FATUMA MTEMANGANI
Wakazi wa kijiji cha safari road wilayani ulanga mkoani morogoro wameaswa kutunza vyanzo vya maji,kuchemsha maji pamoja na kutumia dawa ya kutibu maji kabla ya kunywa ilikuepukana na magonjwa ya milipuko.
Akizungumzia utunzaji wa maji hayo afisa afya wilaya ulanga bwana samson mweta amesema kua kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo wananchi wanatakiwa kuchemsha maji safi na salama.
Hata hivyo bwana mweta amebainisha kuwa kwa wale wote wanaokiuka utunzaji wa vyanzo vya maji watachukuliwa hatua kwa mijibu wa sheria ndogo za halmashauri za usafi wa mazingira ambazo zimeanza kutumika tangu mwezi wa kumi .
Wilaya ya ulanga ni miongoni mwa wilaya zinazokabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kutokana na maeneo mengine kukumbwa na mafuriko ambayo yamesababisha uharibifu wa miundo mbinu ya maji pamoja na wakazi kufanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji .
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.