Wanawake wilayani ulanga mkoani Morogoro wanatarajia kupatiwa elimu kwa kuzimbua fursa zilizopo katika maeneo yao kwa kukitumia vyema chombo cha wanawake wilayani ulanga.
Akizungumza na Redio Ulanga Fm mwenyekiti wa chombo hicho bi.Jasmin Kihele amesema kua uwepo wa chombo hicho utasaidia kuwaunganisha wanawake walio mijini na vijijini ili kuibua fursa za kiuchumi na namna sahihi ya kupambana na dhana ya wanawake kutopendana.
Bi.Kihele ameongeza kua lengo kuu la kuanzisha chombo hicho ni wanawake kukaa pamoja na kupanga mikakati ya kua walinzi na kutoa ushirkiano kwa baadhi ya watu wanaowapa mimba mtoto wa kike pamoja na kumkomboa kuhakikisha hakatishi ndoto zake ili atimize malengo yake aliyokusudia.
Aidha watapatiwa elimu juu ya kukatishwa tamaa katika jamii,kudhurumiwa,kutopea nafasi katika kusimamia mirathi pamoja na kupata sauti ya pamoja ili kutekeleza haki zao kwa kupitia chombo cha wanawake Wilayani Ulanga.
Chombo cha Wanawake wilayani Ulanga kimebeba kauli mbiu isemayo WANAWAKE TUZUNGUMZE na kinatarajia kuzinduliwa rasmi hivi karibuni wilayani ulanga mkoani Morogoro kwa lengo la kuondoa dhana ya wanawake kutopendana.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.