Wanufaika wa mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) wamewashauri wenzao kutotumia fedha wanazopewa katika ulevi badala yake wazitumie katika kujiinua kiuchumi.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa zoezi la ugawaji wa fedha hizo katika vijiji tofauti ndani ya wilaya wamesema kuwa baadhi ya wenzao hutumia fedha hizo kwa kununulia pombe ambapo ni kinyume na madhumuni ya serikali inayowataka kutumia fedha hizo kujikwamua kiuchumi.
Wameongeza kuwa wengi wao wamenufaika na wameinuka kiuchumi kutokana na fedha hizo na kuanzisha biashara ambazo zinawasaidia kuingiza kipato kwa ajili ya kuendesha maisha ya familia nzima.
”Naishukuru sana serikali kwa fedha zao kwani mimi ni mjane mumewangu alifariki aliniacha kwenye nyumba ya nyasi lakini baada ya kuanza kupata fedha hizi nimejenga nyumba nyingine ya bati na kuanzisha ufugaji wa nguruwe na ninapata fedha ya kuihudumia familia.”Alisema bi Servina Eligati mmoja wa wanufaika kutoka kijiji cha Isongo.
Bi Servina aliongeza kuwa pamoja na kutumia kwenye ulevi pia wanaotumia fedha hizo kwa ununuzi wa sigara wanapaswa kuacha kwani nayo ni matumizi mabaya ya fedha hizo na kuwashauri kuzingatia madhumuni ya fedha hizo zinazotolewa kwao na serikali.
Zoezi la ugawaji wa fedha za ruzuku kwa kaya maskini wilayani Ulanga limefanyika katika vijiji mbalimbali ambapo jumla ya vijiji 31 kati ya 59 vinanufaika na fedha hizo zenye lengo la kuwainua mwananchi kiuchumi.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.