Wananchi wilayani Ulanga wametakiwa kuwa na desturi ya kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kwani sasa sio tamko tena ni sheria inayotambulika.
Kauli hiyo imetolewa leo na Afisa Mazingira na Usafi Wilayani Ulanga Bw. Jastin Bundu wakati akitoa tathmini ya usafi wa mwisho wa mwezi Septemba na kuonekana na idadi ya watu wanaoshiriki zoezi la usafi wanazidi kupungua siku hadi siku.
Bwana Bundu amesema kuwa wao wamejipanga kuanzia mwisho wa mwezi huu wataanza kutoza faini za papo kwa papo kwa wale wote wataoshindwa kushiriki kufanya usafi katika maeneo yao kwani kwasasa ni sheria inayotambulika.
Aidha amewataka wananchi wote Wilayani Ulanga kujitokeza kwenye usafi huo pia kuhakikisha mazingira yao wanayoishi yanakuwa safi muda wote sio mpaka kusubiria usafi wa jumuiya ndipo wafanye usafi.
Zoezi la usafi liliagizwa na Mh. Rais John Magufuli kuhakikisha kila mazingira wanayoishi watanzania na taasisi zinakuwa safi muda wote.
Mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.