ULANGA
Na Fatuma Mtemangani
Wazazi na walezi Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro wametakiwa kutoa ushirikiano kwa walimu kujua na kusimamia maendeleo ya wanafunzi ili kuongeza ufaulu na kuepusha wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika.
Hayo yameelezwa na Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Ulanga Bwana Benard Lupenza wakati akizungumza na Redio Ulanga FM juu ya wanafunzi wanaorudishwa madarasa kutokana na uwelewa wao katika masomo kuwa mdogo.
Aidha ndugu Lupenza amezitaja sababu zinazosababisha wanafunzi hao kurudishwa madarasa ni kuwa na uwelewa mdogo katika kupokea masoma pamoja na ushirikiano mdogo wa wazazi kwa walimu kwani wazazi wanaoshirikiana nao vizuri watoto wao wanafanya vizuri kimasomo.
Hata hiyo amewataka wazazi na walezi kuhudhuria mikutano ya shule pindi wanapo hitajika shuleni ili kujua mustakabali wa watoto wao.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.