Na . Yuster Sengo
Mkuu wa shule ya sekondari ya Nawenge iliyopo Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro Bi. Magret Duncan Lwisa ametoa wito kwa Wazazi kuwasimamia wanafunzi ipasavyo na kuwatimizia mahitaji yao ili waweze kufikia malengo yao kielimu.
Akizungumza shuleni hapo mkuu huyo wa shule amesema kuwa ili kufanikisha malengo ya wanafunzi ni wajibu kwa wazazi kuwasimami vizuri watoto wao kwa kushirikiana na walimu ili kuhakikisha wanafunzi hao wanapewa uangalizi pindi wawapo shuleni na hata majumbani.
“Jukumu la kuwasimamia watoto ni la wote ,walimu wanawasimamia wanpo kuwa shuleni na wanapokuwa nyumbani jukumu hilo linakuwa la wazazi/walezi ,hivyo tunapaswa kulifanya hilo kwa uhakika ili kuwasaidia watoto wetu kwenye suala zima la elimu”Amesema Mkuu wa shule
Pia Bi. Magret ameongeza kuwa kwenye shule ya Sekondari Nawenge ipo mikakati kadhaa ya kuhakikisha wanafunzi wanafaulu kama ulivyo mpango wa shule ambapo katika kulifanikisha hilo Walimu wamekuwa wakiwafuatilia kwa ukaribu wanafunzi hao ili kujua changamoto zao na kuzitatua.
Kwa upande wake Mwalimu wa Taaluma shuleni hapo Bw. Festo Kawamala amewashukuru walimu wote shuleni hapo kwa kuendelea kushirikiana na ofisi ya Taaluma na kujituma katika kazi yao ili kufanikisha shule hiyo kuendelea kupata matokeo mazuri.
Aidha Mkuu wa shule hiyo ameiomba serikali kuongeza idadi ya Walimu shuleni hapo ili kuwapunguzia mzigo walimu waliopo kwani kutokana na uchache wao wamekua wakifanya kazi kubwa ili kufikia malengo ya shule.
Kwa upande wa matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka huu Shule ya Sekondari Nawenge imefaulisha Wanafunzi wote kwa madaraja tofauti ambapo idadi ya Wanafunzi waliopata daraja la kwanza ni 44, daraja la pili ni wanafunzi 80, daraja la tatu ni wanafunzi 5 na hakuna Wanafunzi waliopata daraja la nne na sifuri.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.