Na .Erasto Liwemba
Kila octoba mosi ni siku ya wazee duniani, wazee wa wilaya ya ulanga wametembelea kituo cha watoto yatima kilochopo ukwama kwaajili ya maathimisho ya siku hiyo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “kuzeeka kwa usawa” hivyo basi wazee wilayani Ulanga wameamua kutembelea watoto yatima kituo cha Ukwama na kutoa chochote kitu.
Akizungumza kwenye maadhimisho haya, muwakilishi wa wazee Joseph Mphalashi amesema kufanya hivyo ni kuonesha mapenzi kwa watoto wanaoshi kwenye Maisha magumu na hatarishi.
Mzee mphalashi ameogeza kwa kusema “tumeamua kuwatembelea Watoto yatima kutokana na ushauri tuliopata kutoka kwa ustawi wa jamii wilayani ulanga hivyo basi nawashukuru wazee wenzangu waliojitokeza siku hiyo”.
Mlezi wa kituo hicho Mama Choma amesema “faraja kwetu kutembelewa na wazee kwenye siku ya maadhimisho pia tunashukuru kupata mchango mkubwa wa chakula kutoka kwa wazee wetu na mungu awalinginde awape Maisha malefu”
Monica Bayi ni afisa ustawi wa jamii wilayani Ulanga amewasiku wazee kwa kuwa na moyo wa kujitoa kusaidia Watoto yatima.
Aidha afisa huyo amesema kuwa “nawashukuru wazee kwa kuwa na moyo mzuri kwa kujitoa ili kufanikisha swala hilo kwani wangeamua kutumia hela yako ili kukuza mfuko wao lakini wameamua kuwasaidia Watoto yatima siku ya leo”
mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.