Na Yuster Sengo
Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dk Merdad Kalemani ameitaka Tanesco wilayani Ulanga kufikisha umeme katika migodi ya Epanko ili kuwasaidia wachimbaji wa mgodi huo kuchimba kwa tija na kupata faida itakayowawezesha kulipa kodi kwa serikali na waweze kujiinua kiuchumi
Hayo ameyasema tarehe 23 february 2021 wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Ulanga ya kutembelea migodi ya Epanko na kuangalia jinsi ya kufikisha miundombinu ya umeme katika Kijiji hicho cha Epanko
“Meneja wa Tanesco wa Wilaya , wiki ijayo muanze kupeleka umeme katika migodi hiyo , utamwambia Meneja wako wa mkoa ambaye tupo naye hapa akupe shilingi milioni mia nne kwaajili ya kupeleka umeme huku migodini “Amesema Mh kalemani
Aidha ameongeza kuwa kwa kufikisha umeme katika migodi hiyo ya Epanko kutasaidia kuweza kupata kodi ya serikali kwani kwa mwezi migodi hiyo inauwezo wa kukusanya shilingi miliomi tano ambapo ndani ya miezi michache tu inaweza kupatikana shilingi milioni mia nne ambayo ilitumika kwaajili ya kupeleka umeme
“ kwanza nashangaa kwanini tulikiuwa hatujaleta umeme kwakuwa hawa wachimbaji tukiwafungia umeme kwa mwezi tunaweza kupata shilingi milioni tano ambapo ndani ya mwezi mmoja tunarudisha milioni mia nne tuliyoiwekeza hapo”Amesema Mh Kalemani
Hata hivyo amemtaka mkuu wa wilaya ya Ulanga Mh.Ngollo Malenya kuchukua hatua pale atakapo ona kuwa kazi hiyo ya kupeleke umeme ina rega rega
“Mkuu wa wilaya ukiona kazi ina rega rega kamata meneja wa Tanesco wa wilaya weka ndani,na huyu wa mkoan nita shughulika nae mimi,pia kamata kandarasi weka ndani naamini REA wanaingia ubia na suma JKT kwahiyo kazi itaenda kwa kasi na kukamilika kwa wakati”Ameongeza waziri wa Nishati Mh Merdad Kalemani
Aidha ameagiza vijiji vyote vilivyofikiwa na miundombinu ya umeme vilipie ili viunganishiwe umeme kwa haraka na kuanza kufaidi matunda ya serikzli ya awamu ya Tano
Kwa upande wa mbunge wa Ulanga Mh,Salim Alaudin Hasham amesema kuwa anaishukuru seriklai kwa kujipanga kufikisha umeme kwenye vitongoji vyote na pia amemshukuru Mh.Medrd Kalemani kufika katika eneo hilo la migodi ya epenko kwaajili ya kuangalia uhitaji wa umeme katika eneo hilp
‘Mimi nimshukuru sana Waziri wa Nishati kwa kufika hapa ,lengo ilikuwa ni kufika migodini kuangalia shughuli tunazofanya lakini kuokana na hali ya hewa pamoja ni barabara kutokupitika kwaajili ya mvua zinazo endelea kunyesha ameshindwa kufika huko lakini ameahidi kuleta umeme katika eneo hilo la Epanko”Amesema Mh.Mbunge wa Wilaya ya Ulanga
“Nimshukuru pia Mh.Rais kwakuhakikisha kuwa nchi yetu inapata maendeleo,na ninafahamu kuwa serikali imejipanga kuwa vitongoji vyote Tanzania nzima vinaenda kupata umeme kwani kuna vilio vingi vya umeme kufika barabarani na huko ndani ndani unakuwa haujafika “Ameongeza Mh.Salim
Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji ,Bw Joseph Mpandule amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa kuwa namba moja ya chachu ya maendeleo hasa vijijini
Mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.