Na .Yuster Sengo
Maonesho ya 27 ya wakulima nane nane yamezinduliwa rasmi leo tarehe 1/8/2020 katika viwanja vya mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika manispaa ya Morogoro
Akihutubia wakati wa zoezi la ufunguaji rasmi wa maonesho ya nane nane mwaka 2020,mgeni rasmi katika sherehe hizo waziri wa mambo ya nje Mh Palamagamba Kabudi amesema kuwa maonesho ya mwaka huu ni ya kipekee kwasababu yanafanyika kipindi ambacho dunia imekumbwa na janga la ugonjwa wa corona lakini kwa namna ya pekee Tanzania imeweza kuhimili hali hiyo
”nichukue nafasi hii kumshukuru Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mh.dk John Pombe Magufuli kwa namna alivyo shughulikia jambo hili la covid-19 na hadi leo tunaendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa ikiwa ni pamoja na kushiriki maonesho kama haya
Amesema tumefanikiwa hayo kwasababu ya uongozi madhubuti wa Mh ,Rais ,lakini pia kwa watanzania kuonesha nidhamu ya juu ya kutekeleza yale yote waliyoambiwa kuhusu tahadhari ya kupambana na ugonjwa huo
“kunawa kwa maji safi na sabuni,lakini pia kujifukiza kwa mimea mbali mbali ambayo mwenyezi mungu ameitengeneza,na leo katika maonesho haya kuna banda nimetembela na kuukuta ule mmea uliotusaidia sana kipindi cha mapambano ya corona mmea huo unaitwa kifumbasi”ameongeza Mh. Waziri Palamagamba Kabudi
Aidha ameongeza kuwa mkoa wa Morogoro umechangia sana kwa uzalishaji wa tangawizi na limao ambazo zilitumika kwa kiwango kikubwa sana wakati wa mapambano ya janga la covid -19
“niwashukuru sana wakulima wa tangawiz na limao i kwa jambo kubwa walilolifanya ,na tusilichukulie kama jambo dogo ,wakulima wa tangawizi nchini mwaka huu wametoa mchango mkubwa ambao umetunusuru na covid 19,na kikubwa hawakupandisha bei ya tangawizi wala limao
Aidha ameongeza kuwa sasa ni wakati muafaka kwa watanzania kuanza kulima miti dawa au mimea dawa kwani ndani ya miaka mitano ijayo ,miti dawa na mimea dawa itakuwa ni biashara kubwa sana duniani kote
Awali akisoma taarifa ya maandalizi ya nane nane kanda ya mashariki inayo jumuiya mikoa minne ambayo ni Tanga, Morogoro ,Pwani na Dar es salaam katibu tawala wa Tanga amesema kuwa kwa mwaka huu wa 2020 maandalizi ya nanenane yalichelewa kuanza kutokana na sababu mbali mbali
”kwa mwaka huu maandalizi ya nane nane kanda ya mashariki yalichelewa sana kuanza kwasababu ya changamoto ya janga la ugonjwa wa wa corona ulioukumba nchi yetu pamoja na ulimwengu kwa ujumla , lakini tunamshukuru Mungu kwa kuinusuru nchi yetu na janga hili la corona
Aidha ameongeza kuwa kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu inayosema kwa maendeleo ya kilimo,mifugo na uvuvu ,chagua viongozi bora 2020,kanda ya mashariki maonesho haya yameshirikisha washirika wa taasisi za umma na sekta binafsi ili kutoa elimu na kufanya wakulima ,wafugaji na wajasiriamali kujifunza mbinu mbali mbali na teknolojia mpya za kuendeleza shughuli zao za kiuchumi
Hata hivyoameongeza kuwa jumla ya washiriki 526 wamejiandikisha kushiriki katika maonesho haya ukilinganisha na washiriki 512 kwa mwaka jana nab ado tunaendelea kuwapokea washiriki wengine kwakuwa maonesho hayo ndo kwanza yameanza
Aidha amemuomba mgheni rasmi kuwasaidia ili mwakani maonesho ya nane nane kitaifa yafanyike kanda ya mashariki katika viwanja vya mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Maonesho ya sherehe za nane nane kwa mwaka 2020 imepambwa na kauli mbiu inayosema ,KWA MAENDELEO YA KILIMO ,MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.