Na. Yuster Sengo
Mafunzo ya mfumo wa anwani za makazi na jinsi zoezi hilo litakavyo fanyika limekamilika kwa kutoa mafunzo kwa wenyeviti wa vijiji pamoja na maafisa watendaji kata na vijiji katika tarafa za vigoi , lupiro ,ruaha na mwaya
Mafunzo hayo yaliyofanywa katika tarafa hizo lilikua na lengo kubwa la kuwajengea uwezo katika kusimamia zoezila anwani ya makazi na post kodi
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika mafunzo hayo ,mratibu wa zoezi hilo bw . Loius Ndumbaro amewataka wajumbe hao kuwa wasikivu katika mafumzo hayo kwani zoezi hilo ni kitaifa na linatakiwa kufanywa haraka na kwa uhakika ili kufikia lengo lengo lililo wekwa
Aidha ameongeza kuwa zoezi hilo litafanyika kwa kubainisha majina ya mitaa na barabara kwa kushirikisha wananchi kwani zoezi linahusu watu wote .
Kufanyika kwa zoezi hili kutafanya serikali kuwa na takwimu sahihi ya maeneo yanayoitaji huduma za kijamii kama vile afya elimu na miundombinu pamoja na urahisishaji upelekaji wa mizigo /vifurushi hadi kwa watu husika kwa kutumia anwani iliyoandikwa kwenye mzigo huo
"kila mtanzania atakuwa na anwani halisi ya makazi yatakayomsaidia kila mtu kupatikana kiurahisi. hivyo zoezi hili litarahisisha kufikiwa na mizigo au bidhaa tunazoagiza badala ya kuzifata katika stendi ya mabasi kwani anwani yako itamfikisha mtu anayekuletea mzigo wako kwa urahisi
Uelimishaji huo umekamilika katika tarafa zote za wilaya ya ulanga , ikiwa tayari mafunzo hayo yameshafanyika kwa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya ulanga ,wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ili kuweza kuwajengea uwezo juu ya zoezi hilo
Mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.