Ulanga
na Fatuma Mtemangani
Wilaya ya Ulanga ni miongoni mwa wilaya zilizofanya vizuri kwa matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2017 kwa kushika nafasi ya pili kwa mkoa wa morogoro.
Hayo yamebainishwa na afisa elimu sekondari bw.Menard Lupenza wakati waziara ya mkuu wa wilaya ya Ulanga kukagua ujenzi wa madarasa ya wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Vigoi.
Bw.Lupenza ameongeza kua ili kuwe na ufaulu mzuri wazazi na walezi wanatakiwa kushirikiana kujenga hostel na kuchangia chakula kwa ajili ya wanafunzi wanaotembea umbali mrefu kufuata elimu hali inayopelekea wengine kukatisha ndoto zao kwa ajili ya vishawishi pamoja na kutofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha nne.
Hata hivyo kwa wilaya ya Ulanga kuna baadhi ya shule za sekondari zikikabiliwa na changamoto ya vyumba vya madarasa kumi na tano meza pamoja na viti ikiwemo Mbuga Sekondari , Ilonga Sekondari,Ulanga Sekondari,Mahenge Sekondari pamoja na Vigoi Sekondari.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga nduguYusuf Semuguruka ametoa wito kwa viongozi wa kata na vijiji kutowachangisha wazazi juu ya ujenzi wa shule hizo kwani kwa kufanya hivyo ni kukiuka tamko alilotamka mh.Raiswa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dk.John Pombe Mgufuli kuwa elimu ni bure.
Aidha mkurugenzi Semuguruka amewataka viongozi wa kata, vijiji na vitongoji kuacha siasa na badala yake wafanye kazi kwa kushirikiana na wananchi kwa kuchangia shilingi elfu tano kwa kila nguvu kazi kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa madarasa hayo ifikapo tarehe 8/1/2018 ili wanafunzi wa kidato cha kwanza waweze kusoma kwani maendeleo sio ya chama bali ni ya watanzania wenyewe.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.