20/10/2017 JUKWAA LA WANAWAKE
Wanawake wilayani Ulanga Mkoani Morogoro uenda wa kakuwa zaidi kiuchumi na kupunguza vitendo vya ukatili dhidi yao endapo wataungana na kulitumia vyema jukwaa la wanawake.
Afisa maendeleo ya jamii wilayani Ulanga bi.Jackline Mpongoliana amesema kua uwepo wa jukwaa hilo utasaidia kuwaunganisha wanawake na kuibua fursa za kiuchumi na namna sahihi ya kupambana na vitendo vya ukatili dhidi yao.
Bi. Mpongoliana ameongeza kua wanawake wana nguvu kubwa ya kusimamia masuala ya maendeleo lakini wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kutozitambua fursa zilizopo katika maeneo yao,kukatishwa tama na baadhi ya wanaume,kudhurumiwa,kutopewa nafasi katika kusimamia mirathi pamoja na kukosa sauti ya pamoja ya kutekeleza haki zao.
Katika kukabiliana na changamoto hizo ofisi ya maendeleo ya jamii kwa kuwatumia wataalamu kutoka taasisi za kifedha ikiwemo benki na taasisi mbalimbali za maendeleo imeanza zoezi la uchaguzi kwa ngazi ya kata kuchagua viongozi ikiwemo mwenyekiti,katibu na muweka hazina kwa kila kata.
Aidha jumla ya kata 21 zilizopo wilayani Ulanga kata takribani 15 zimeshafanya uchaguzi na kuwapata viongozi wa kata na zoezi hilo linasimamiwa na maafisa watendaji kata,waheshimiwa madiwani pamoja na viongozi kutoka Halmashauri huku kata zilizosalia linaendelea na uchaguzi.
Hata hivyo taasisis hizo pia kwa kuwatumia wataalam wake wanatoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake juu ya masuala ya maendeleo pamoja na kuzitambua fursa zilizopo katika maeneo yao pamoja na kupata sauti ya pamoja ili kutekeleza haki zao.
Jukwaa la wanawake limezinduliwa rasmi wilayani Ulanga tarehe 27/4/2017 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali lililotolewa na makamu wa rasi Samia Suluhu Hassani la kutaka kila wilaya kuunda jukwa la wanawake.
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.