Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya ulanga ndugu yusuf semuguluka amewaagiza maafisa watendaji kata, maafisa watendaji vijiji pamoja na maafisa ugani wa mifugo kutoa taarifa kwa wafugaji ili juu ya zoezi la kubaini idadi ya mifugo inayohitaji kupigwa chapa.
Akizungumzia zoezi hilo mkurugenzi semuguluka amesema kua zoezi hilo litahusisha wafugaji wa asili,mifugo iliyopigwa chapa ikafutika pamoja na wale ambao hawakusajili mifugo yao kuwasiliana na viongozi wa vijiji na kata ili mifugo yao iweze kupigwa chapa.
Hata hivyo kwa wale wafugaji ambao waliopiga chapa mwaka 2016 mpaka mwaka 2017 vitambulisho vyao vimekamilika hivyo gharama ya chapa ni sh.500 na kwa ngombe aliyefutika chapa atarudia kupigwa chapa bure.
Aidha mkurugenzi ameongeza kua viongozi hao wanatakiwa kuandaa ujenzi vibanio vya kupigia chapa mahali ambapo zoezi hilo litafanyika hivyo mfugaji wa ngombe za asili ahakikishe kua mifugo yake inapigwa chapa.
Zoezi la kupiga chapa mifugo wilayani ulanga litaanza rasmi tarehe 7/03/2018 na kukamilika tarehe 28/03/2018 na kwa mfugaji ambae hajasajili mifugo yake hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kuzuia mifugo yake kuuza mnadani,kuchinja machinjioni,pamoja na kutopatiwa kibali cha kusafirishamifugo yake.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.